Back to top

POLISI WATOA MSAADA WAZEE WASIOJIWEZA NJORO

06 March 2025
Share

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kilimanjaro (SP) Asia Matauka ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoani humo, ameitaka Jamii kudumisha upendo kwa kujitoa ili kujenga ushirikiano.

Amesema hayo wakati wakati mtandao wa Polisi wanawake (TPF-net) mkoani humo kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha wazee wasiojiweza  Njoro, kilichopo Kata ya Mji mpya mkoani humo na kusisitiza jamii kuonyesha matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji kwa kujitoa hata kwa kidogo walichonacho kwani ni baraka mbele za Mungu hasa katika kipindi hiki cha mfungo.

Amewashukuru askari Polisi wanawake mkoani humo kwa umoja wao kwa kutenga muda na kutembelea wazee hao, jambo linaloonesha upendo na inajenga taswira nzuri kwa Jeshi la Polisi kushiriki shughuli za kijamii.

Vitu vilivyotolewa ni mchele kilo 100, unga wa ugali kilo 50, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kula lita 20, miswaki katoni 1, dawa ya meno katoni1, mafuta ya kupaka katoni 1, sabuni ya unga mifuko 2, miche boksi 2,  mifagio 4, pampasi 7, sabuni ya maji lita10, majani ya chai dazeni 1, wembe dazeni1, sukari kilo 25, chumvi katoni 1, vifaa vya usafi brashi za chooni 4 pamoja na mopa 4