Back to top

RAIS MWINYI AMEKUTANA NA MWAKILISHI MPYA UNICEF

21 August 2023
Share

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeeleza dhamira yake ya kuboresha na kuendeleza huduma za jamii kwa wananchi wake, ikiwemo kuimarisha huduma za afya, elimu, maji safi na salama na kudumisha usafi wa mazingira.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi mpya wa Taasisi ya Hifadhi ya Watoto ya Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia masuala ya Elimu na Watoto duniani, (UNICEF) Bi. Elke Wisch aliyefika kujitambulisha.

Naye, Mwakilishi huyo wa UNICEF, Tanzania Elke Wisch alishukuru ushirikiano uliopo baina ya UNICEF na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye ustawi wa masuala ya watoto na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.