Back to top

RAIS SAMIA APONGEZWA UJENZI WA DARAJA LA PANGANI

26 February 2025
Share

Wakazi wa Wilaya ya Pangani wamempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ujenzi wa daraja la Pangani pamoja na utekelezaji wa miradi mingine Wilayani humo ikiwemo miradi ya maji, shule, afya na ujenzi wa josho la mifugo kwa ajili ya jamii ya wafugaji lenye thamani ya shilingi milioni 38.

Daraja hilo litaunganisha barabara ya ushoroba wa Pwani inayoanzia eneo la Malindi, kwenda Hororo- Bagamoyo - Tanga, ambapo linatarajia kurahisisha usafirishaji mazao ya biashara na chakula pamoja na kuchochea utalii na uchumi wa Buluu na kuondoa changamoto ya wakazi wa Pangani  kutegemea kivuko MV Tanga pekee kuvuka mto Pangani.

Ujenzi wa daraja hilo umetoa fursa ya ajira kwa vijana wa Mkoa wa Tanga na baadhi ya Mikoa jirani ambapo wanajipatia fedha za kujikimu kwa ajili yao binafsi na familia zao.

Rais Dkt. Samia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 ambalo thamani yake ni shilingi bilioni 82.