Back to top

RAIS WA CAMEROON AONEKANA BAADA YA KUZUSHIWA KIFO

22 October 2024
Share

 Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 91 ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza ndani ya wiki sita huku kukiwa na uvumi kuhusu afya yake kudorora.

Kutokuwepo kwake hadharani kulisababisha uvumi usio na msingi wa kifo chake. Lakini siku ya Jumatatu mchana televisheni ya taifa ilionyesha picha za kuwasili kwa rais huyo katika uwanja wa ndege kwenye mji mkuu Yaoundé, kwa ndege kutoka Uswizi.

Serikali ilikuwa imepiga marufuku vyombo vya habari kujadili afya ya Biya – ambaye amekuwa madarakani tangu 1982 - ikiainisha kama suala la usalama wa taifa.

Tetesi za kifo chake zimekuwa zikienea kila mara kwa miongo miwili iliyopita.