Back to top

Robo ya watu walioambukizwa Ugonjwa wa Ebola Congo DRC hawajui.

08 June 2019
Share

Shirika la Afya Duniani limesema karibu robo ya walioambukizwa Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hawajui wanaugua ugonjwa huo.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake kuwa mtu mmoja kati ya wanne Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ameambukizwa ugonjwa hatari wa ebola lakini hafahamu.

Limesema inaendelea kusaidia kupambana na maambukizi ya ebola hasa mjini Beni, ambako watu zaidi ya elfu mbili wameambukizwa na wengine elfu moja mia tatu hamsini na saba wamefariki dunia tangu Agosti mwaka 2018.

Aidha, hivi karibuni Jumuiya ya Afrika Mashariki ilihadahrisha kuhusu tishio la ugonjwa huo kuenea katika nchi za jumuiya hiyo.