Back to top

RUTO AONYA WALIOFADHILI MAANDAMANO KENYA

26 June 2024
Share

Rais wa Kenya, William Ruto amewaonya wapangaji wa Maandamano, wafadhili, wanaochochea ghasia na machafuko nchini humo na kusema maandamano yaliyofanyika ni kama uhaini hivyo serikali haitosita kuwachukulia hatua watakaobainika.

Rais Ruto amenyooshea kidole pia waliohusika katika uvamizi wa Bunge nakubainisha kukabiliwa kisheria, na kwamba ameamua kuchukua Jeshi kusaidiana na polisi nchini kote ili kukabiliana na dharura ya usalama iliyosababishwa na maandamano, yaliyopelekea watu kufariki dunia na wengine kujeruhiwa wakati wa kupinga muswaada wa fedha wa mwaka wa 2024. 

Wengi wa waliojeruhiwa wanapata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.