Back to top

RUVUMA: TANESCO WAKABIDHIWA GARI LA KUBEBEA NGUZO

20 July 2024
Share

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga, amekabidhi gari la kubebea nguzo katika Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma. 

Mhe.Kapinga amesema Serikali itaendelea kuboresha maslahi, vitendea kazi na mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi wa TANESCO ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumzia changamoto ya kukatika kwa umeme wilayani Mbinga, Kapinga amesema Serikali imeshaweka mikakati ya kujenga kituo kipya  cha umeme ambacho kitaboresha hali ya upatikaji umeme,ambapo amewahakikishia wananchi kuwa kituo hicho cha kupokea na kupooza umeme kitajengwa katika mradi wa Gridi imara awamu ya pili.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO  Wilaya ya Mbinga, Mhandisi Edward Kweka, amesema kuwa walikuwa wakikutana na changamoto ya ubebaji nguzo, kutokana na kutokuwepo kwa gari la kubebea nguzo hizo,hivyo gari hilo litawasaidia kutoa huduma kwa ufanisi na kuahidi kulitunza.