
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amesema moja ya majukumu yatakayotekelezwa na Baraza la Michezo, katika mwaka wa fedha 2024/25, ni pamoja kuanzisha safari ya Tanzania kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2030.
.
Dkt.Ndumbaro ameeleza hayo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025, ambapo ametaja majukumu mengine ni pamoja na kutekeleza mkakati maalumu wa kulea timu za vijana, kuwa na timu za vijana chini ya miaka 17 ambayo itatokana na mashindano ya UMITASHUMTA, chini ya miaka 20 ambayo itatokana na mashindano ya UMISETA, na chini ya miaka 23 ambayo itatokana na wachezaji wanaocheza Ligi, wasio kwenye Ligi na Diaspora walioko nje ya nchi.
.
"Baraza la Michezo, katika mwaka wa fedha 2024/25, majukumu yatakayotekelezwa ni pamoja na kuendelea kuwezesha na kuzigharamia timu za Taifa katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa...kuanzisha safari ya Kombe la Dunia, mwaka 2030, kwa sababu tumeamua kama Tanzania kwa muongozo wa Mhe.Rais tunataka tukacheze Kombe la Dunia mwaka 2030" ameeleza Dkt.Ndumbaro.
