Back to top

Serikali kufanya ukaguzi wa kina wa miradi mbalimbali ya maji.

23 May 2019
Share

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kufanya ukaguzi wa kina wa miradi mbalimbali ya maji nchini ili kubaini utekelezaji wake kama umefanyika katika viwango vilivyokusudiwa na ile ambayo itakuwa imefanyika chini ya kiwango waliohusika watawajibishwa.

Mh Majaliwa ameyasema hayo bungeni leo wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu.

Kiongozi huyo akaongeza kuwa ni kweli ipo miradi mingi ya maji na utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua na ndio maana kuna hatua mbalimbali ambazo mpaka sasa hivi zimechuliwa ili kukabiliana na changamoto zilizoko katika miradi hiyo.

Aidha Mh Waziri mkuu ametolea ufafanuzi masuala mengine ikiwemo kilimo na migogoro ya ardhi na hatua tofauti tofauti ambazo zimechuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa ili kuweka mambo sawa.