Back to top

Serikali kutumia utaratibu wa nguvu kazi kuliko wa zabuni.

22 November 2019
Share

Rais wa Tanzania Mhe.John Magufuli amesema utaratibu wa kutumia nguvu kazi badala ya wakandarasi umekuwa chachu ya serikali kuokoa fedha katika ujenzi.

Dkt.Magufuli amesema hayo mkoani Dodoma wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 118 ambapo amesema Serikali itauendeleza  utaratibu huo wa nguvu kazi kuliko ule wa kutoa zabuni kwa wakandarasi.

Awali Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Kangi Lugola amesema wizara hiyo kupitia taasisi zilizo chini yake imefanikiwa kutatua  matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakizikabili taasisi hizo.

Rais Magufuli yuko katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.