Back to top

Serikali yatenga milioni 871.98 kukamilisha miradi ya maji.

24 June 2019
Share

Naibu waziri wa maji Mhe.Juma Aweso amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 871.98 kwa ajili ya kuendelea kukamilisha miradi ya zamani ya maji na miradi mipya.

Akijibu swali la mbunge wa Rufiji Mhe.Mohamed Mchengerwa aliyehoji ni lini serikali itatatua kero ya maji katika kata ya Ngarambe, Mbwala, Chumbi,Muholo na maeneo mengine mbalimbali ya Tarafa Ikwilili kwa kuchimba visima.

Mhe.Aweso amesema serikali inatambua changamoto ya huduma ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Rufiji na kwa sasa tayari baadhi ya kata hizo zimeanza kupewa kipaumbele cha kujengewa miradi ya maji.

Amesema katika Kata ya Chumbi vimechimbwa visima viwili ambapo kwa sasa vipo katika hatua ya usanifu wa mradi, ambapo katika kata ya Muholo imewekwa kwenye utekelezaji wa miradi ya awamu ya pili ambapo tayari usanifu wa mradi umekamilika.