Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda, amesema suala la amani ni jambo ambalo linatakiwa kushirikisha Jamii, ili amani na utulivu wa eneo husika uimarike, kutokana na ushiriki kamili wa wananchi katika ulinzi wa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi, kwani suala la amani ya eneo husika linatakiwa kuanza na Jamii husika.
CP Kaganda amesisitiza kuwa suala la Polisi jamii ni njia nzuri, katika masuala ya ulinzi wa amani kutoka na tafiti alizozifanya na uzoefu wake akiwa Mkuu wa operesheni za kulinda amani katika eneo la Abyei Sudan Kusini.
CP Kaganda amebainisha haya wakati wa mafunzo kwa askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani, yanayoendelea Chicago Nchini Marekani, ambayo yamejumuisha nchi zaidi ya sitini na nne ambapo ametoa uzoefu wake katika masuala ya Polisi Jamii na namna ambavyo wananchi wanaweza kushiriki kulinda amani ya eneo husika bila ya kuwa na Jeshi la Polisi wala Jeshi lolote katika eneo lenye changamoto ya amani.
Mbali na hilo washiriki wengine kutoka Nchini Tanzania, wameeleza namna mafunzo hayo yalivyowaimarisha katika kujiamini, kiutendaji na nafasi wanazopewa hudumu huku waki weka wazi kuwa pindi watakaporudi nchini Tanzania watanzania wategemee mabadiliko makubwa kutokana mafunzo hayo.
Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Johari Saidi yeye akaeleza namna mafunzo hayo yalivyowapa mwanga katika mgawanyo wa majukum bila kuathiri familia walizonazo ikiwa ni pamoja na namna Bora ya utunzaji wa afya kwa askari kutokana na unyeti wa majukum makubwa waliyonayovyombo vya ulinzi.