Back to top

TAARIFA YA UKOPAJI IKICHAFUKA KUSAFISHWA NI MIAKA 6

26 February 2025
Share

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuwa kwa mtu yeyote anayekopa na kutorejesha kwa wakati mkopo alio kopa taarifa zake huwasilishwa katika kanzidata kama mkopoji sugu mwenye mkopo chechefu na atafungiwa kupata huduma hizo kwa miaka sita hadi kusafishwa.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha, Deogratius Mnyamani, wakati Akiwasilisha mada ya mafanikio na changamoto za usismamizi wa sekta ya huduma ndogo za fedha, amesema kila mmoja ana historia ya ulipaji wa mikopo lengo ni kujia tabia ya urejeshaji wa mikopo na kwmaba mitandao yote ya simu imeingia kwenye mfumo huo.

“Rekodi yako ikishachafuka kuisafisha ni miaka sita mbele, achana na uliyochafuka kwa makosa ya bahati mbaya kwamba ulishalipa ila mtoa huduma akuiweka vizuri, na kama si mlipaji mfumo unakwenda kadi kwenye kodi ya ardhi na ankra za maji,utaonekana hujalipa,”amesema.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa ukiona muda wa kulipa deni umefika  amewashauri wakopwaji wasizime simu au kuhama mtaa, bali watoe taarifa kwa mtoa huduma ajue sababu za kutetereka na sababu hizo zinaweza kuwa biashara kuteteraka ukame, magonjwa ya mlipuko n.k, kisha baada yah apo mteja na mtoa huduma mtakubania endapo mtoa huduma ataelewa sababu zako namna ya kuliweka vizuri deni husika.