Back to top

TAKUKURU kuwafikisha Kisutu watumishi 3 waliomba rushwa ya milioni 2

10 June 2019
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo itawapndisha Mahakamani watumishi watatu waliohusika na ukamataji na uuzaji wa mizigo ya Mfanyabiashara Ramadhani Hamisi Ntunzwe kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni mbili.

Watuhumiwa hao watatu watafikishwa katika Nahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa hilo la kuomba rushwa ya shilingi milioni mbili kutoka kwa mfanyabiashara huyo wana Ramadhani Hamisi Ntunzwe kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

TAKUKURU imesema imebaini kwamba watuhumiwa hao waliomba kiasi hicho cha fedha kwa mfanyabiashara huyo kama kishawishi ili aweze kuachia mzigo wa mfanyabiashara huyo ambao waliukamata kwa madaui ya kufanya udanganyifu wa kiwango bidhaa alizonazo.