Back to top

TANESCO: TATIZO SIO LUKU NI MAPUMZIKO YA DISEMBA

04 January 2024
Share

Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limesema malalamiko ya baadhi ya wateja wake kuhusu mita za LUKU kuonekana kutumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi yao kwa miezi ya nyuma, haitokani na ubora wa mita hizo, bali inatokana na sababu zingine mbalimbali, zinazochangia ongezeko hilo, ikiwemo mapumziko ya miezi ya Disemba na Januari, ambayo watu wengi wanakuwa nyumbani katika mapumziko ya mwisho wa mwaka, hivyo kusababisha matumizi mengi ya vifaa vya umeme.  
.
Kupitia taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na Shirika hilo imebainisha kuwa mita za LUKU zina ubora wa hali ya juu unaokubalika kwa viwango vya kimataifa vilivyothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kwamba ili kuthibitisha ubora na usahihi wa mita hizo kabla hazijatumika kwa wateja, Shirika hilo hufanya uhakiki wa ufanisi ili kujiridhisha.