
Wakazi wa Jiji la Tanga wafurahishwa na ziara ya Rais Mhe. Dkt. Samia Mkoani Tanga, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara ya kikazi Jijini humo tangu aingie madarakani.
Wakazi hao wamempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia kwa kuazimia kuleta mabadiliko ya kimaendeleo Jijini Tanga kwa Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kujenga viwanda, vyuo vikuu, hoteli za kitalii na utalii wa ufukweni, lengo likuwa ni kuliinua kiuchumi Jiji hilo.
Ahadi za kuleta mabadiliko hayo zimetolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia wakati akiwahutubia wakazi wa Jiji la Tanga katika uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga.