Back to top

TANZANIA INA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

01 March 2025
Share

 Mmiliki wa Kampuni ya Usambazaji Gesi ya GBP Badar Soud, amewashauri wawekezaji kuja Nchini Tanzania kuwekeza katika miradi ya Sekta mbalimbali. 

Akizungumza baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Ujenzi wa LPG Terminal GBP Gas Tanga,  Badar Soud, amesema wamevutiwa na kupata matumanini ya kuwekeza Nchini Tanzania kutokana na Sera nzuri na rafiki za Uwekezaji za Serikali ya awamu ya sita.

Mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu dola za Marekani Milioni 50 na utatoa ajira zisizopungua 1,000.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa GBP, Billal Juma amempongeza Rais Dkt. Samia kwamba kupitia wawekezaji wanaokuja Nchini inasaidia wananchi kupata ajira zinazowawezesha kumudu maisha yao ya kila siku.