Back to top

Tanzania yatumia bilioni 400 ikiagiza mafuta ya kula toka nje.

29 April 2019
Share

Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga, amesema Tanzania imekuwa ikitumia shilingi bilioni 400 kwa mwaka  kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa mbegu za mafuta za kutosha huku mwaka huu zikitumika zaidi ya shilingi bilioni 650 kuagiza bidhaa hiyo.

Kufuatia hali hiyo Taasisi ya utafiti wa kilimo nchini (TARI)imeanza mikakati ya kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa kuzalisha mafuta ya kupikia hapa nchini kwa kukuza kilimo cha mbegu kitakachosaidia kuzaliza mafuta yanayotokana na mazao ya ufuta, michikichi,alizeti, karanga pamoja na minazi ili kukidhi soko la mafuta ya kula.