Back to top

TAWIRI NA KOREA KUSINI KUENDELEZA UHIFADHI

18 March 2025
Share

Timu ya Watafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) na timu ya Wataalamu kutoka Korea Kusini kupitia  Taasisi ya Bioanuai ya Korea Kusini (NIBR) inatarajia kuingia uwanda wa kaskazini mwa Tanzania, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu katika tafiti za utambuzi wa bioanuai za mimea, wadudu, ndege na wanyama wadogo hapa nchini.

Mtafiti kutoka TAWIRI Dk. Bukombe John, amesema utambuzi wa bioanuai ni muhimu kwani kutokana na mabadiliko mbalimbali ya tabia nchi na ongezeko la  binadamu  hupelekea baadhi ya bioanuai  kuwa katika hatari ya kutoweka, hivyo kwa kuzitambua na kuanisha mahali zinapopatikana inasaidia kutoa ushauri wa namna ya kuhifadhi bioanuai hizo. 

Aidha, Dk. Bukombe amesema ushirikiano kati ya TAWIRI na Korea Kusini umekua na tija ikiwemo kuanzishwa kwa chumba maalum cha kuhifadhi bioanuai za wadudu, mimea, ndege na na wanyama wadogo. Chumba hicho hutumiia kwa utafiti na kutoa elimu kwa wadau mbali mbali.