Back to top

"TLS INAHITAJI MTU ANAYEWEZA KUFANYA MAAMUZI" NKUBA

28 July 2024
Share

Joto la nani atakuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) limezidi kupanda kutokana na mchuano mkali wa wagombea unaoendelea hivi sasa kuelekea siku ya Uchaguzi wa Rais wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 Agosti 2024 katika ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Akiongea kwenye mjadala wa wagombea wa Urais wa chama hicho, Wakili Sweetbert Nkuba mmoja wa Mgombea wa Urais wa TLS amesema chama hicho kinahitaji mtu ambaye anaweza kufanya maamuzi na kuwa na msimamo wa kusimamia kile ambacho TLS imeundwa kwa ajili yake.

Wakili Sweetbert amesema kuwa na mahusiano na wadau sio udhaifu hivyo chama hicho kinahitaji kuwa na mahusiano bora na Serikali, Jeshi la Polisi na Mahakama 

Amesisitiza jambo lingine ni kuhakikisha kazi za mawakili zinapatikana kwa namba yoyote ile wadau wanaotakiwa kutoa kazi za mawakili wazitoe sambamba na kusimamia madhumuni ya TLS  kama yalivyoainishwa kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya chama hicho ikiwa ni pamoja kuhakikisha TLS inakuwa bingwa wa kusimamia haki za mawakili na haki za Jamii.