Back to top

TNMC: WAKUNGA, WAUGUZI ZINGATIENI HAKI NA USALAMA

19 June 2024
Share

Wauguzi na Wakunga wametakiwa kuzingatia haki, usalama, kuheshimu imani, mila na desturi ambazo haziathiri utoaji wa huduma za kiuuguzi na Ukunga. 

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Usajili, leseni  na Maadili kutoka Baraza la Uuguzi na ukunga Tanzania, Bi.Jane Mazigo, wakati wa utoaji wa mafunzo  ya kuhamasisha maadili, Sheria ya Uuguzi na Ukunga na huduma bora kwa wateja Mkoani Tanga.

Pamoja na shughuli hizo Maafisa kutoka TNMC, watatembelea vyuo vya Uuguzi na Ukunga ili kujionea hali halisi ya utoaji wa Mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kusisitiza uzingatiaji wa miongozo.