Back to top

TRUMP KUBADILI HOTUBA, BAADA YA KUEPUKA 'KIFO'

15 July 2024
Share

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, amewasili Milwaukee kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Kitaifa la Republican, ambapo anatarajiwa kupokea uteuzi rasmi wa chama hicho kwa kinyang'anyiro cha urais wa 2024 pamoja na kumtangaza mgombea mwenza.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema baada ya jaribio la kutaka kuuawa siku ya Jumamosi,  anaandika tena "hotuba kali sana" kuhusu "utawala mbaya" wa Biden aliokuwa ameitayarisha kwa hafla hiyo, akitarajia kuunganisha nchi.

Donald Trump anasema "ataileta nchi pamoja" katika kongamano la Chama cha Republican wiki hii, baada ya kuponea chupu chupu katika jaribio la mauaji siku ya Jumamosi.

Siku ya Jumapili usiku, Rais Biden alitoa hotuba kwenye televisheni, ambapo alitoa wito wa  "joto la siasa" kupunguzwa huku akitaka Wamarekani kuacha kugeuza siasa kama uwanja wa vita.

Katika hotuba yake, Joe Biden kwa mara nyingine tena ametoa rambirambi zake kwa familia ya Corey Compatore, mtu aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi katika kampeni ya Trump.

Mtu aliyejaribu kumuua Trump - Thomas Crooks, 20 - alipigwa risasi na kuuawa na Wahudumu wa siri, lakini nia yake bado haijajulikana.