Back to top

Ubanguaji  korosho wa mtu au vikundi utambuliwe.

02 February 2022
Share

Bodi ya Korosho Tanzania imeshauriwa kuandaa mfumo utakaotambua korosho zinazobanguliwa na mtu mmoja mmoja ama vikundi, ili ziweze kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa takwimu za mauzo ya korosho kwa kila msimu ambazo kwa sasa takwimu hizo hazipo.

Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Patrick Sawala aliyemwakilisha mkuu wa mkoa katika Mkutano  wa Tathmini wa zao la Korosho ulioshirikisha mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Tanga, Ruvuma na Pwani inayolima zao hilo.

Amesema wakati umefika kwa Bodi ya Korosho kukaa pamoja na viongozi wa halmashauri  zinazolima zao la Korosho, ili kuweka mfumo utakaowezesha korosho zote za wabanguaji wadogo zinaingia kwenye mfumo wa mauzo ya stakabadhi mazao ghalani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho nchini Francis Alfred amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathimini ya msimu uliopita na kupanga mikakati yenye tija katika uzalishaji wa zao la korosho kwa msimu wa mwaka huu wa 2022/2023.