Back to top

UHAMIAJI NA CHANGAMOTO, ZAMULIKWA MAREKANI

03 September 2024
Share

Mafunzo kwa Shirikisho la askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani yameendelea katika Jiji la Chicago Nchini Marekani, ambapo suala la wahamiaji na changamoto zake kutokana na mabadiliko ya Sheria baina ya Nchi na Nchi, likamulikwa na washiriki wakapata nafasi ya kubadilisha uzoefu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Tatu Burhan, amesema kuwa masomo waliojifunza yamejikita katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa na utatuzi wa changamoto za wahamiaji wanaoingia katika mataifa mbalimbali, na namna bora ya kuzitatu changamoto hizo.

Ameongeza kuwa masomo hayo waliofundishwa yamewapa namna bora ya kukabiliana changamoto za wahamiaji ambao wamekuwa wakiingia katika nchi tofauti tofauti kwa lengo la makazi akaweka wazi kuwa suala la wahamiaji ni suala mtambuka linalotegemea sera zitakazoleta mabadiliko ya kukabiliana na changamoto za wahamiaji wanaoingia katika mataifa husika.

Aidha DCI Tatu akabainisha kuwa mafunzo waliyoyapata pia yamewakumbusha suala la matumizi ya teknolojia ili kukabiliana na wahamiaji ambao wanaingia katika nchini bila ya kufuata taratibu ambapo alisema kuwa zipo sababu zinazomfanya mtu kuingia katika nchi husika, huku akitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watanzania kuendelea kushirikiana na idara hiyo katika kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Nae Mkufunzi Kutoka Wizara ya  huduma za Binadamu Chicago ambaye aliyetoa mada na mafunzo ya masuala ya mipaka na wahamiaji Bwana Ronald Vitiello akaeleza namna alivyoweza kubadilisha uzoefu na washiriki wa mafunzo hayo katika jiji la Chicago ambapo amesema mafunzo hayo yalikuwa ni juu ya changamoto za mipaka katika maeneo ya Marekani na Mexico na mipaka kwa ujumla.

Ronald akaweka wazi kuwa wamejadiliana na kubadilisha uzoefu akieleza mgogoro baina ya Marekani na Mexico na athari zake kwa uhusiano na ushirikiano wa kimataifa Pamoja na sheria za upelelezi.

Mafunzo hayo yanaendelea huku mada mbalimbali zikifundishwa ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji washriki wa mafunzo hayo hayo ambayo kidunia yanafanyika Chicago Nchini Marekani yakihisha Mataifa zaidi ya siti na Nne.