
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Nishati, Bi.Anita Ishengoma, amesema katika utekelezaji wa majukumu ya kisekta Wizara ya Nishati imetoa fursa za usawa kwa wanawake.
Bi.Ishengoma ameyasema hayo katika kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 Machi ambapo nchini, itaadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.
Amesema kuwa uwepo wa uwiano wa jinsia unatoa fursa sawa kwenye maamuzi katika ngazi za juu katika kutekeleza majukumu ya kisekta.
Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ameasa Wanawake kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo.