Back to top

V8 YAKAMATWA IKISAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU

08 April 2024
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewakamata watu 17  ambao ni raia wa Ethiopia, kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kutokuwa na vibali.
.
Akitoa taarifa hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Lucas Mwakatundu, ameeleza kuwa watu hao wamekamatwa katika Kijiji cha Kiongozi, kilichopo wilayani Babati, wakisafirishwa kwenye gari aina ya V8 VXR yenye namba bandia za serikali, STL 1964, huku dereva wa gari hilo akikimbia baada ya kugundua kuwa anafuatiliwa na Polisi.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limewaomba  wananchi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Polisi ili kuhakikisha hakuna magendo yanayopitishwa kwa kutoa taarifa za watuhumiwa wa uhalifu.