Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima amewaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini kuhakikisha majengo ya vituo vya afya na zahanati ambavyo havijakamilika vifunguliwe mara moja na vianze kutumika kwa kutoa huduma muhimu zikiwemo chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano wakati serikali ikikamilisha ujenzi wa vituo na zahanati hizo.
Dokta Gwajima ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya chanjo dunia ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Morogoro katika shule ya msingi Chamwino B manispaa ya Morogoro.