Back to top

Wakulima wa viazi mviringo Makete walia na soko.

16 November 2019
Share

Baadhi ya wakulima wa viazi katika kijiji cha Ukange wilaya ya Makete mkoani Njombe ambao ni wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)  wamelalamikia upatikanaji wa soko la viazi.

Wakulima hao zaidi ya 70, ambao wamewezeshwa na TASAF vifaa mbalimbali vya umwagiliaji ikiwemo mabomba, kupitia mpango wa TASAF wanazalisha viazi kwa wingi tofauti na mwanzo lakini changamoto kubwa ni soko la kuuzia zao hilo.

Wakati baadhi ya wakulima wakilia na soko la viazi hivyo lakini pia baadhi yao wameishukuru serikali kuwawezesha kilimo hicho na kwamba kimeondoa hali ya udumavu katika jamii.