Back to top

Waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege walipwa wilayani Songea

15 October 2019
Share

Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni  mia sita kuwalipa fidia wananchi 162 walioondolewa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma unaojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 37 na kampuni ya kichina ya Chico.

Hayo yameelezwa na meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) wa mkoa wa Ruvuma mhandisi Razeck Alinanuswe wakati akiwaeleza wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya mkoa huo maendeleo ya mradi huo

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amesema kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika Disemba 28 mwaka 2020 utavutia mkoa wa Ruvuma kiuchumi kwa kuwa utaruhusu ndege kubwa kutua na kwamba hawatarajii malalamiko ya fidia.