Back to top

WANACHAMA PSSSF KUHUDUMIWA KIDIJITALI

29 August 2024
Share

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetehamisha huduma zake kutoka matumizi ya karatasi kwenda PSSSF Kidijitali, ambapo mwanachama atatumia Simu janja au Kompyuta kupata huduma zote zinazohusiana na uanachama wake.


Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Bw.Venance Mwaijibe, amebainisha hayo wakati wa utoaji huduma kwa wajumbe wa Kikao Kazi cha Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma, ambacho kimefunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).


"Pamoja na kutoa huduma kwa wanachama, jambo kubwa tunalofanya hapa ni kuwaelimisha jinsi ya kutumia simu janja kupata huduma hizo ikiwemo, kupata taarifa za michango, taarifa za mafao, kuwasilisha madai mbalimbali, lakini na wastaafu nao wanaweza kujihakiki" Bw.Mwaijibe.