Back to top

WANACHAMA WAVUTIWA NA HUDUMA YA PSSSF KIDIGITALI

01 July 2024
Share

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umesema kumekuwa na muituikio mzuri wa Wanachama kutumia mtandao kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko.

Akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere, maarufu viwanja vya Sabasaba, jijini Dar Es Salaam, Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Bi. Rehema Mkamba, amesema “Kwa sasa tunasema PSSSF Kidijitali zaidi, tunawahamasisha wanachama wetu kutumia PSSSF Kiganjani Mobile App na PSSSF Member Portal ulipo Mtandaoni, ili kupata huduma zinazotolewa na Mfuko bila ya Mwanachama kufika kwenye ofisi za PSSSF.”

Miongoni mwa Wanachama wa PSSSF waliofika katika banda la PSSSF na kufurahiswa na huduma ya  PSSSF Kidijitali  ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere.

Akiongozwa na Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Bw. Abdul Njaidi na Afisa Huduma kwa Wateja Bi. Nahira Mang’ana, Bw. Kichere alioyeshwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF Kidijitali, ambapo kupitia simu yake aliweza kuskani QRCORD ya PSSSF Kiganjani Mobile App.