Wakati msimu wa kilimo ukiwa umewadia mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mgema amewaonya watu wanaowarubuni wakulima kwa kuwakopesha mbolea kwa makubaliano ya kinyonyaji ya mfuko mmoja wa mbolea kwa malipo ya magunia manne ya mahindi baada ya mavuno.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wakulima wa kijiji cha Lusonga na kuongeza kuwa njia pekee ya kuepukana na hujuma hiyo ni kujiunga na vyama vya ushirikahuku akiwataka wanaowarubuni wakulima kuacha tabia hiyo.
Naye afisa wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA katika mkoa wa Ruvuma Bi. Laika Nasoro anasema kuwa mtandao huo umejikita kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima ili wakulima walime kilimo biashara na si kilimo cha kuhami njaa.