![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/ajali%20bahi.jpg?itok=pE-zeWsu)
Watu watano wamefariki na wengine 14 wamejeruhiwa usiku wa kuamkia leo kufuatia ajali ya Basi dogo la abiria lililokuwa limebeba abiria 19 waliokuwa wakitokea kwenye sherehe ya harusi eneo la Makanda wilayani Manyoni mkoani Singida kuelekea Bahi mkoani Dodoma kugongana na Trekta.
Kwa upande wake muuguzi mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Bw.Stanley Mahundo amesema mpaka sasa hospitalini hapo wamebaki majeruhi wanne huku mganga mkuu wa kituo cha afya Bahi Dkt.Honest Kasasa amesema wamepokea majeruhi 14 na miili mitano kutoka kwenye eneo la ajali.
Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amewaasa askari wanaohusika na ukaguzi wa magari kuhakiki usajili wa vyombo pamoja na ubora wake.