#HABARI: Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda amesema Tanzania haikuchaguliwa kwa bahati mbaya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, isipokuwa imekidhi vigezo ambavyo waandaji wamejiridhisha navyo.
Ameeleza haya jijini Dar es Salaam, na kwamba pamoja na Tanzania kuwa moja ya nchi chache za Afrika zenye mipango thabiti ya kuwa na nishati ya kutosha na uhakika, mpango wa kusambaza umeme nchi nzima Vijiji na Vitongoji na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kinara wa kuhamasisha matumizi ya nihati safi ya kupikia, mikakati kabambe ya upatikanaji wa nishati ambapo malengo ifikapo 2030 asilimia 75 ya Watanzania wawe wamefikiwa na umeme na asilimia 80 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034,
Sababu nyingine alizozitaji kuwa ni kuimarika kwa diplomasia ya Tanzania, amani na usalama na uzoefu wa kutosha wa kuwa nwenyeji wa mikutano mikubwa ambayo imekuwa ikifanyika nchini.
Mkutano huo unaondaliwa kwa ushirikiano baina ya Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Tanzania unalenga kuwakutanisha wakuu wa nchi zote za Afrika na wadau wengine ili kujadili kwa pamoja njia za kuchagiza upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu kwa kutumia rasilimali zilizopo.