Back to top

Watu 1900 wathibitishwa kuugua ugonjwa wa Dengue nchini.

16 May 2019
Share

Watu 1900 wathibitishwa kupata virusi vya ugonjwa wa Dengue nchini.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa serikali Prof.Muhammad Bakari Kambi amesema kuwa idadi hiyo ya wagongwa wa Dengue kati yao 1800 wanatoka Dar es Salaam ambapo wengine tayari wamepona na wengine bado wanatibiwa katika hospitali na vituo vya afya nchini.

Prof.Kambi ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa watu 75 huambukizwa ugonjwa wa Dengue kila siku toka watu 32, na kufanya maambukizi mapya kufikia watu 674.

Aidha amefafanua kwamba ugonjwa huo mpaka sasa hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja na kuwasihi wananchi kuwa makini na baadhi ya watu wanaojifanya wanatibu ugonjwa huo kwani watambue ugonjwa huo hauna tiba.