Back to top

MAJAHAZI 2 YAKAMATWA NA SHEHENA YA MAFUTA DAR

29 June 2024
Share

Jeshi la Polisi Kikosi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam, kimefanikiwa kukamata majahazi mawili, MV.UKIMAINDI POA na Jahazi lingine lisilokuwa na jina wala namba za usajili katika Bahari ya Hindi, Dar es Salaam, yakiwa na watuhumiwa wanne akiwepo Nahonda Masoud Rajabu wakiwa wamebeba mafuta ya kupikia dumu 1731 zenye ujazo wa lita 20 kila moja wakiwa na nia ya kukwepa ushuru wa forodha.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji ACP Moshi Sokoro, amesema Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi, umebaini watuhumiwa hao hawakuwa na nyaraka zinazothibitisha uhalali wa umiliki wa mizigo hiyo ya mafuta ya kupikia pamoja na nyaraka za usafirishaji.

Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wafanyabiashara wasio waadilifu kuacha mara moja, kusafirisha mizigo kwa njia ya bahari bila kuwa na nyaraka za mizigo hiyo, na pia kwa wavuvi haramu na wamiliki wa boti pamoja na manahodha wanaobeba abiria kwa boti ambazo sio salama maeneo ya feri Kigamboni na feri Magogoni kuacha tabia hiyo kwani Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua.