Back to top

WAZIRI MKUU KATIKA MAZIKO YA BABA WA KATIBU MKUU KIONGOZI.

16 October 2024
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika maziko ya Mzee Jeremiah Kusiluka ambaye ni Baba mzazi wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka yaliyofanyika katika kijiji cha Madihani, Makete mkoani Njombe.

Akitoa salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu za msiba huo na waendelee kumuombea marehemu Mzee Jeremiah ili Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kuyaenzi mema yote aliyoyafanya marehemu kipindi cha uhai wake. “Tuenzi yale yote mema aliyoyafanya mzee wetu Jeremiah wakati wa uhai wake, tukifanya hivyo tutakuwa tumetenda haki. ”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi wanatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kutokana na msiba huo.
 
Akizungumza kwa Niaba ya Familia, Prof. Lughano Kusiluka ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kushiriki wake katika kumuaga Mzee Jeremiah. “Asanteni kwa kuja kushiriki nasi, tunawashukuru sana kwa kutuunga mkono kuja kushiriki nasi katika kumuaga mzee wetu, heshima hii ni kubwa na haielezeki. ”

Aliongeza kuwa Mzee Jeremiah alikuwa ni Baba imara na mwenye msimamo. “Mara zote alitusisitiza lazima tuheshimu watu tufanye kazi ili tuweze kuishi na alitukumbusha kuwa hapa katika kijiji cha Madihani, Kipahalo ni nyumbani kwetu. ” Alisema.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka amesema kuwa Marehemu Mzee Jeremiah alikuwa ni mpenda maendeleo na watoto wake wote wamekuwa wakienzi msimamo huo. “Pamoja na kuwa mpenda maendeleo pia baba alikuwa mchaMungu na ameondoka akiwa mchaMungu. ”

Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kutokana na historia ya mzee Jeremiah hasa kwenye malezi ya watoto wake inapaswa kusherehekea maisha yake kwa kuwa anakuwa shujaa wa Makete na Tanzania kwa ujumla. “Mafanikio ya watoto wake katika utumishi wa umma hayana kificho. ”
 
Viongozi walioshiriki msiba huo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonaz, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Antony Sanga, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Msajili wa Hazina Nehemia Kyando Mchechu