Back to top

Waziri Mpango aagiza taasisi za fedha kudhibiti utakatishaji wa fedha.

09 July 2019
Share

Waziri wa fedha na mipango Dk. Philip ,Mpango ameziagiza taasisi za fedha zote kushirikiana na vyombo vya dola katika kudhibiti utakatishaji wa fedha haramu kupitia mabenki huku akizitaka taasisi hizo za fedha kutoa taarifa mapema za miamala inayotia mashaka ili kuzuia vitendo vya kiuhalifu vinavyofanywa katika baadhi ya benki hapa nchini.

Dk.Mpango ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akikabidhiwa gawio la shilingi bilioni 1.2 kwa serikali pamoja na wanahisa wengine wa Benki ya Posta Tanzania kama faida ambayo wameipata kutokana na shughuli zake ambapo amesema swala la utakatishaji wa fedha haramu bado ni changamoto ambapo amesema serikali kupitia vyombo vya dola inaendelea kusaka wahalifu.

Aidha katika hatua nyingine Dk. Mpango amezitaka taasisi za fedha kuhakikisha zinawasaidia watanzania kujikwamua na hali ya umaskini kwa kuwakopesha mikopo yenye riba nafuu hali itakayosaidia kuinua uchumi wa nchi.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo, Dk Edmund Mndolwa amesema benki ya TPB inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kufikia uchumi wa kati ambapo amewataka watanzania kutumia taasisi za fedha ikiwemo kukopa fedha kwa ajili ya kupaata mitaji ya biashara.