Back to top

Waziri Mpina awataka wafugaji kutumia mifugo waliyonayo kusomeshea.

01 September 2018
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina ameelekeza jamii za wafugaji nchini kutumia fursa ya mifugo waliyo nayo kusomesha watoto na kuchangia ujenzi wa hosteli za watoto wakike katika kila shule ya sekondari lengo likiwa ni kutatua na changamoto ya mimba kwa wanafunzi wakike hali ambayo inasababisha wasichana wengi kukatisha masomo yao.

Waziri Mpina ametoa kauli hiyo wakati akipokea michango ya wa nanchi wa wilaya ya Simiyu waliojitolea kujenga hosteli ya wanafunzi wakike katika shule ya sekondari katika wilaya ya simiyu ambayo imebaki na wanafunzi 19 wa kidato cha nne baada ya wengine kuacha masomo kutokana na sababu tofauti tofauti ikiwemo wazazi kuhama hama na mifugo na wene kupata ujauzito.