Back to top

Waziri wa Ulinzi wa Urusi aitahadharisha Marekani.

19 August 2019
Share

Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Jererali Sergei Shoigu ametahadharisha kwamba, nchi yake itajibu hatua yoyote ya Marekani ya kuweka makombora katika nchi za Asia na Ulaya.

Jererali Shoigu amesema nchi hiyo inataka kufanya mazungumzo na Marekani na haitafanya lolote kama marekani haitaweka Asia la Ulaya makombora yanayokiuka mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF).

Ameongeza kuwa, mwaka mmoja kabla ya Marekani kujiondoa katika mkataba huo, Marekani ilitenga fedha za kuunda makombora ya masafa ya kati na masafa marefu katika bajeti yake ya masuala ya ulinzi.

Amesisitiza kuwa Urusi iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani kuhusiana na makombora ya masafa mafupi na masafa ya kati.

Kadhia ya makombora ya masafa mafupi na ya kati imekuwa maudhui muhimu zaidi inayozusha hitilafu baina ya Urusi na Marekani na imeibua mvutano mpya kati ya nchi hizo mbili.

Mapema mwezi huu Marekani ilitangaza rasmi kujitoa katika mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya 0Kati (INF).