![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/SHUKURU%20r.jpg?itok=3l8Su2UG)
Klabu ya soka ya Yanga SC imemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaandalia hafla ya kuwapongeza kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika la CAF, iliyofanyika jana Juni 05, 2023, ikulu mkoani Dar es Salaam.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, pia imemshukuru Rais Samia kwa hamasa yake ya 'Goli la Mama' aliyoitoa kwa klabu hiyo kuanzia hatua za makundi hadi fainali na kuifanya timu hiyo kujipatia Tsh. Mil. 135 kwa magoli 17.