Back to top

AJALI YA BASI YAUA WANNE TANGA

03 October 2024
Share

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 Kujeruhiwa baada ya basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha kupata ajali ya kuacha njia na Kupinduka katika eneo la Maili kumi, barabara ya Segera-Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea Octoba 3, 2024, majira ya saa 7 na nusu usiku, ambapo basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Julias Mushi (43) mkazi wa Arusha.

Kamanda Mchunguzi ametoa onyo kwa madereva kufuata Sheria za barabarani nyakati zote kwa kuchukua tahadhari na kuheshimu sheria za usalama Barabarani kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho wa Safari.