Back to top

MLEZI AWANYANYASA WATOTO KINGONO NA KUWAREKODI

03 October 2024
Share

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Teresia Wambui Kihagi mlezi wa kituo cha kulea watoto katika soko la Wangige, Kaunti ya Kiambu huko nchini Kenya, amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwanyanyasa watoto kingono.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, mlezi huyo alikuwa na zaidi ya watoto 10, ambao wote wanaaminika kuwa waathiriwa wa vitendo vyake viovu.

Wakati akisomewa mashtaka hayo mahakamani siku ya Jumanne, ilibainishwa kuwa mlezi huyo alijaribu kuharibu ushahidi wa video kwa kuponda simu yake.

“Mshtakiwa anadaiwa kuwashirikisha watoto hao wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi minne katika vitendo vya ngono, na kuwashika sehemu zao za siri huku akiwarekodi wakiwa kwenye kitendo hicho kwenye gari,” Maelezo katika hati ya mahakama.

Afisa wa uchunguzi Nicodemus Musembi alisema kuwa uchunguzi utafanywa kwenye nambari zake za simu, ili kubaini wapokeaji wa video hizo na pia kukagua bili ya malipo ya Equity, ambayo amekuwa akitumia katika utunzaji wa watoto.

Mtuhumiwa huyo amezuiliwa kwa siku 21 ili kupisha uchunguzi zaidi, huku akifanyiwa uchunguzi wa kiakili, wakati huo huo, waathiriwa wamepelekwa katika vituo tofauti vya afya kwa uchunguzi wa kimatibabu.