Back to top

UZALISHAJI KAHAWA GHAFI WAONGEZEKA NYANDA ZA JUU

05 October 2024
Share

Wakati Tanzania, ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kahawa Duniani, uzalishaji wa kahawa ghafi kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, umetajwa kuongezeka ambapo zaidi ya Tani 12,000, zimekusanywa kwa mwezi Agosti mwaka huu, huku ubora wa kahawa hiyo aina ya Arabica, inayozalishwa katika ukanda huo ukizidi kuwa na ushindani mkubwa katika soko la kimataifa.
 
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kahawa Duniani kwa Nyanda za Juu Kusini, yaliyofanyika mkoani Songwe, nakukutanisha wadau mbalimbali, Meneja wa Bodi ya Kahawa wa Nyanda za Juu Kusini, Bw. Sijali Bowa, anasema makisio ya uzalisha wa kahawa ghafi kwa msimu wa kilimo kwa mwaka 2024/2025, ilikuwa Tani 16,500.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Bw. Beno Malisa, kwa niaba ya serikali kando na kupongeza jitihada hizo  anawataka wakulima kuendelea kuzingatia ubora wa kahawa hiyo inayotokana na teknolojia mpya ya miche chotara aina ya compact hali ambayo itasaidia kuliteka soko la kimataifa.
 
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ushirikiano wa wadau ndio nguzo endelevu ya zao la kahawa baadhi ya wakulima wameomba serikali kuendelea kufanya utafiti wa zao hilo ili kupata mbegu na miche bora zaidi ambayo itaongeza uzalishaji na kufikia lengo la serikali.