Back to top

MSAADA HOSPITALINI NA KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

12 October 2024
Share

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula kwenye hospitali tatu za Rufaa za Mikoa ya Mbeya, Arusha, Mtwara na Morogoro pamoja na kwa watoto wenye uhitaji maalum. 

Misaada hiyo ambayo imetolewa katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii kutokana na pato la Mfuko.

Hospitali ambazo zimefaidika na misaada hiyo ya PSSSF, ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Meneja wa Pensheni za Wastaafu PSSSF, Bw. Kwame Temu ndiye aliyewasilisha msaada huo maalum kwa wodi ya watoto wenye changamoto ya Lishe.

Kwa upande wa Mkoa wa Arusha, Meneja wa Kumbukumbu za Wanachama Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Edgar Shumbusho, yeye alimkabidhi vifaa tiba, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), Dkt. Alex Ernest.

Wakati Meneja wa PSSSF Mkoani Mtwara, Bw.Say Lulyalya, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mgtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, katika hafla iliyohudhuriwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa, Ligula.

Aidha, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Morogoro, Bi. Zaida Mahava, yeye alikabidhi vifaa vya ujenzi na vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege mkoani humo.