Back to top

MKUU WA KITUO MATATANI KWA KUMVUNJA MKONO RAIA

19 October 2024
Share

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, amesema Jeshi hilo limeshachua hatua dhidi ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Makete, baada ya kulalamikiwa na Levis Mahenge, kuwa alimkamata kisha kumpeleka Kituo cha Polisi na kumpiga hadi kumvunja mkono.
 
DCP Misime amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 9,2024, na baada ya tukio hilo kugundulika na Uongozi wa Polisi Mkoa wa Njombe, jalada lilifunguliwa na ushahidi ukakusanywa na uchunguzi umekamilika.

Kufuatia kitendo hicho hatua za kinidhamu zinaendelea kukamilishwa dhidi ya Mkuu huyo wa Kituo na baadaye hatua za kisheria zitafuata kwa sababu tuhuma anazokabiliwa nazo ni za kijinai.