Back to top

WAKILI WA MGOMBEA URAIS AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

21 October 2024
Share

Wakili wa Kiongozi maarufu wa Upinzani Nchini Msumbiji, Bw. Venâncio Mondlane, ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji Mkuu Maputo pamoja na afisa wa chama chake. Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi Oktoba 19, 2024.

Elvino Dias alikuwa wakili wa Venâncio Mondlane, ambaye aligombea urais katika uchaguzi siku 10 zilizopita, kama mgombea binafsi akiungwa mkono na chama cha siasa cha Podemos.

"Waliuawa kikatili [katika] mauaji ya kinyama," lilisema shirika la haki za mitaa la Kituo cha Demokrasia na Haki za Kibinadamu (CDD).

"Dalili [zinaonyesha] kwamba karibu risasi 10 hadi 15 zilipigwa risasi, na walikufa papo hapo," mkurugenzi wa kikundi hicho, Adriano Nuvunga alisema.

Shirika lingine la waangalizi wa uchaguzi wa Mais Integridade, lilisema mauaji hayo yalipangwa ili kumtisha mtu yeyote anayedai uwazi katika uchaguzi.

Inaelezwa kuwa, Dias alikufa papo hapo, huku Guambe, akifariki kwa majeraha masaa machache baadaye. 

Katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia matukio ya kihalifu yameongezeka katika nchi mbalimbali duniani jambo ambalo linatoa taswira kuwa hata yanayotokea nchini Tanzania ni mwendelezo wa matukio hayo ya kihalifu duniani.