Back to top

UGANDA: LORI LA MAFUTA LALIPUKA, WATU 11 WAFARIKI

23 October 2024
Share

Watu zaidi ya 11 wamefariki dunia, baada ya lori la mafuta, kupinduka na kulipuka karibu na mji mkuu wa Uganda, Kampala, baada ya lori hilo kupoteza muelekeo kutokana na hitilafu ya breki.

Msemaji wa Polisi nchini humo, Patrick Onyango amesema kati ya watu 11 waliofariki, wawili miongoni mwao ni watoto na kwamba waathiriwa waliteketea bila kutambuliwa kufuatia mlipuko huo wa lori.

Onyango ameeleza kuwa licha ya tahadhari wanazo zitoa panapotokea matukio kama hayo, lakini bado watu walionekana wakisogea maeneo hayo kwa lengo la kuchota mafuta, ambapo tukio kama hilo lilitokea nchini Nigeria na kuua zaidi ya watu 140 wakiwemo watoto.