Back to top

TANZANIA IMEKUWA YA 9 MATAIFA YENYE MIUNDOMBINU BORA

04 November 2024
Share

Ripoti iliyotolewa na Mtandao wa Statista huku ikichapishwa na businessinsider, imeeleza kuwa Tanzania imetajwa kuwa ya 9 kati ya mataifa 10 barani Afrika, ambayo yana miundombinu bora zaidi ya barabara.

Taarifa hizi zinakuja ikiwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kuanzia mijini hadi Vijijini.

Uwekezaji huo unalenga kuwarahisishia wananchi, kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji kwa urahisi ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.