Back to top

MITAMBO YA RAIS SAMIA YAREJESHA BWAWA LILILOPOTEA HANDENI

16 November 2024
Share

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bwawa la Maji Kwenkambala lililopo Kata ya Kwediyamba, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambao awali ulikumbana na changamoto kadhaa ikiwamo rushwa na kusimamishwa kwa wasimamizi wa mradi.

Waziri Aweso ameeleza kuwa safari ya kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo haikuwa rahisi lakini sasa ameridhishwa kuona mitambo iliyonunuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa bwawa inatumiwa vyema kutokana na usimamizi mzuri wa mradi huo.

Kutokana na hatua hiyo ameahidi kuleta Shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kuongeza kasi ya utekelezaji wake.

"Nilikuja hapa, hali ilikuwa ngumu sana, unamuuliza.Mkandarasi bwawa lipo wapi, halioni", ameeleza Aweso.

Aidha amesema kuwa atahakikisha watu wa eneo hilo wanapata maji safi na salama, akieleza kuwa juhudi kubwa zimefanyika kuhakikisha maji yanapatikana wilayani Handeni chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.